Guardiola Awakemea Mashabiki Wake na kusema Hatambui Timu Yake.

Pep Guardiola alikasirika na uchezajii wa nyumbani wa Manchester City na kusema hatambui timu yake katika hali ya sasa, licha ya ushindi wa 4-2 dhidi ya Tottenham.

 

Guardiola Awakemea Mashabiki Wake na kusema Hatambui Timu Yake.

City walizomewa nje ya uwanja wakiwa nyuma kwa mabao mawili kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza hapo jana katika Uwanja wa Etihad, wakikabiliwa na kipigo cha tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Aprili 2018.

Mpaka kwenda mapumzika dakika 45 za kwanza Spurs walikuwa wakiongoza mabao 2-0 kabla ya City kurejea na mabao ya haraka haraka ya kusawazisha.

Inakuwa mara ya pili kwa City kutokea nyuma mabao mawili chini na kushinda mechi moja ya ligi msimu huu, baada ya kufanya hivyo dhidi ya Crystal Palace mwezi Agosti.

Guardiola Awakemea Mashabiki Wake na kusema Hatambui Timu Yake.

Wakati ushindi huo umesogeza City ndani ya pointi tano za vinara Arsenal, ingawa walikuwa wamecheza mechi moja zaidi, Guardiola mmoja hakufurahishwa na kile alichokishuhudia dhidi ya Tottenham.

Guardiola ameiambia Sky Sports; “Lazima tujiandae vyema zaidi. Siwezi kukataa jinsi tulivyo na furaha lakini tuko mbali na timu tuliyokuwa nayo, sio katika suala la uchezaji, tulicheza vizuri lakini kuna mambo mengine mengi kama vile ushindani.”

Alipoulizwa ni nini kilikosekana kutoka kwa timu yake, Guardiola alisema: “Shauku, moto na hamu ya kutaka kushinda kutoka dakika ya kwanza. Mashabiki wetu walinyamaza kwa dakika 45. Walizomea kwa sababu tulikuwa tunapoteza lakini kipindi cha pili tulicheza vizuri, tulipata nafasi nyingi zaidi.”

Guardiola Awakemea Mashabiki Wake na kusema Hatambui Timu Yake.

City wameshinda Ligi ya Primia katika misimu minne kati ya mitano iliyopita, huku viongozi wa kushangaza Arsenal wakiwinda taji la kwanza katika kipindi cha miaka 20.

Kikosi cha Guardiola bado kinapaswa kumenyana na Arsenal nyumbani na ugenini, lakini kocha huyo wa Kikatalani anasisitiza kuwa timu yake haitawakamata The Gunners isipokuwa wabadilike.

Guardiola anasema kuwa wana mpinzani katika Arsenal ambaye ana moto. Miongo miwili bila kushinda Ligi ya Primia. Kila kitu kiko sawa katika City lakini wapinzani hawasubiri. Na haitambui timu yake, kwani hapo aawali walikuwa na ari na hamu ya kukimbia. Wako mbali na timu waliyokuwa nayo katika misimu iliyopita.

Guardiola Awakemea Mashabiki Wake na kusema Hatambui Timu Yake.

Hadhani kurudi kutatokea kila mara, na anasema kuwa jana walikuwa na bahati. Ikiwa wanataka kushinda kitu au kushindana, basi kwa kulalamika, kulalamika, kulalamika hakuna nafasi watashinda chochote.

Ni wajibu wake mashabiki wake warudi, anataka mashabiki zake walio hapa sio mashabiki wake wa ugenini, wao ni bora zaidi lakini mashabiki wake hapo. Wanahitaji kuunga mkono kila kona na kila hatua, kwa sababu Tottenham ni moja ya wapinzani wagumu ambao amewahi kukutana nao.

Guardiola Awakemea Mashabiki Wake na kusema Hatambui Timu Yake.

Guardiola angalau alikuwa na furaha zaidi alipoulizwa kuhusu onyesho la Mahrez, ambaye sasa ana mabao 11 ya moja kwa moja dhidi ya Spurs, na kuwafanya kuwa mpinzani wake kipenzi.

City watarejea uwanjani Jumapili kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Wolves, huku mechi hiyo ikianza kabla ya Arsenal kukutana na Manchester United.

Acha ujumbe