Guardiola Azima Tetesi za Kwenda Italia: “Nahitaji Kupumzika.”

Pep Guardiola amepuuza tetesi zinazomhusisha na kazi ya ukocha wa timu ya taifa ya Italia, akisisitiza kuwa hana mpango wa kurejea kufundisha mara moja baada ya kuondoka Manchester City.

Guardiola Azima Tetesi za Kwenda Italia: “Nahitaji Kupumzika.”

Kocha huyo raia wa Hispania alieleza kuwa baada ya karibu miongo miwili ya kuwa kocha, anaamini umefika wakati wa kupumzika na kujikita katika mambo mengine ya maisha yake nje ya soka.

“Sihisi kama kuna jambo lolote ninakolikosa kiakili,” alisema Guardiola, akinukuliwa na IlNapolista.

“Nilianza ukocha nikiwa na umri wa miaka 37, na tangu wakati huo maisha yangu yote yamezunguka soka. Sasa nataka kugundua maisha mengine na kuwa na furaha nikifanya mambo ambayo hayahusiani na soka.”

“Ninaipenda kazi yangu, lakini hufika wakati unahisi unahitaji kupumzika. Labda siku moja nitaamka na kusema, ‘Sawa, nataka kurudi kufundisha tena.’ Nahitaji kufikia hatua ya kuikosa kazi hiyo, na kwa sasa bado sijafikia hisia hizo,” alisema Guardiola.

Guardiola aliongeza kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kutumia muda mwingi zaidi na familia yake, hasa watoto wake pamoja na baba yake mwenye umri wa miaka 95.

Guardiola Azima Tetesi za Kwenda Italia: “Nahitaji Kupumzika.”

“Ninajaribu kuelewa maisha yangu yatakuwaje kuanzia sasa,” aliendelea Guardiola. “Niliamua kuacha kwa sababu nataka kujitunza vizuri zaidi. Nataka kutumia muda mwingi zaidi na watoto wangu pamoja na baba yangu mwenye umri wa miaka 95 ambaye bado yupo nasi. Sasa nina miaka 56, si kijana tena, hivyo mtazamo wako kuhusu maisha hubadilika. Bado ninaendelea kuzoea sura hii mpya ya maisha, lakini mambo yanaenda vizuri.”

Kauli zake zinaonekana kuondoa uwezekano wa Guardiola kuchukua nafasi ya ukocha wa timu ya taifa ya Italia (Azzurri) katika kipindi cha karibu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.