Guardiola: De Bruyne Anaweza Kucheza Dhidi ya Arsenal

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amedokeza kua kuna uwezekano wa kiungo wake muhimu ndani ya kikosi chake Kevin de Bruyne anaweza kuwepo kwenye mchezo dhidi ya Arsenal Jumapili.

Kiungo Kevin de Bruyne alipata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Inter Milan siku ya Jumatano na kushindwa kumaliza mchezo huo, Hivo kudhaniwa anaweza kukosekana kwa muda kidogo kutokana na majeraha ambayo ameyapata na mchezo ambao unafuata ni dhidi ya klabu ya Arsenal.guardiola

Pep Guardiola“Kevin de Bruyne anajisikia kidogo vizuri leo, lakini bado… anaweza kushiriki dhidi ya Arsenal.”

“Siku za mapumziko na kesho ni mazoezi, tutaona.

Kutokana na kauli ya kocha huyo inaonesha wazi kua kiungo Kevin de Bruyne anaweza kuwepo kwenye mchezo dhidi ya Arsenal kwakua anaendelea vizuri mpaka sasa, Tofauti na matarajio ya wengi ammbapo ilidhaniwa amepata majeraha makubwa ambayo yangemfanya kushindwa kucheza mchezo huo siku ya Jumapili.

Acha ujumbe