Kocha wa klabu ya Manchester Pep Guardiola ameweka wazi kua kiungo wa kimataifa wa Uingereza Kalvin Phillips alikua tayari kubaki ndani ya klabu hiyo licha ya kutopata dakika nyingi za kucheza.
Kiungo Kalvin Phillips amekua hapati muda wa kucheza zaidi ndani ya kikosi cha Manchester City chini ya kocha Guardiola lakini amemua kusalia ndani ya klabu hiyo, Kocha huyo ameweka wazi klabu ilizungumza na kiungo huyo lakini aliamua kusalia City.Kocha Guardiola anasema kiungo huyo atakua baba karibuni hivo alihitaji kubakia ndani ya timu hiyo, Kwani ni sahihi pia huku akiongeza pia kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza ni mtu mzuri.
Kiungo Kalvin Phillips amekua hapati nafasi mara kwa mara ndani ya kikosi cha City kutokana na majeraha ambayo amekua akiyapata mara kwa mara tangu ajiunge ndani ya timu hiyo akitokea klabu ya Leeds United katika majira ya joto mwaka 2022.Kiungo huyo ameamua kusalia ndani ya klabu hiyo akiamini anaweza kupata dakika za kutosha kwa wakati huu, Kwani anaweza kupambania namba ndani ya timu hiyo kama atakua hana majeraha ya mara kwa mara kama ambavyo yamemtesa kipindi cha nyuma.