Guardiola Kubadili Mfumo wa Uchezaji Kwenye Manchester Derby

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kuwa anakusudia kubadili mbinu kwenye mchezo wa jumapili dhidi Manchester united ili kuzui mashambulizi ya kushitukizi kwenye derby ja jiji la Manchester.

Pep Guardiola anajulikana zaidi kwa mchezo wake wa kumiliki mpira zaidi ila kwenye mchezo wa Manchester derby amepanga kubadilika na kutotumia mfumo wake wa kawaida na amepanga kucheza kwa mfumo wa kushambulia kwa kushitukiza.

Guardiola

Kwenye mchezo wa mwisho ambapo Man City walikaribishwa kwenye dimba la Old Trafford kikosi cha Pep Guardiola kilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, huku kwenye michezo mitatu ya mwisho kwa Man Utd kwenye dimba la Etihad amefanikiwa kushinda mara tatu zote.

Pep Guardiola kwenye mkutano na waandishi wa habari hii leo alinukuliwa akieleza mipango yake ya mchezo huo wa jumapili ambao watawakaribisha Man Utd, “ni kweli tumeshinda sana kwao kuliko kwetu, lakini hakuna sababu maalum kwa hilo.

“Hiyo huwa inatokea, lakini michezo yote tulikuwa tunaangalia zaidi kushambulia na tuliadhibiwa kwa mashambulizi ya kushitukiza, huo ndio uimara wao na ubora wao,  Cristiano, Elanga, Rashford na Sancho wanapopata nafasi ya kukimbia basi huwezi kuwazuia.

“Wana kasi na wako haraka ndio maana tunakwenda kuzuia kwa dakika 90 kwa mara ya kwanza na tutawashambulia kwa kushitukiza nasi.”


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

Acha ujumbe