Pep Guardiola atasimamia mchezo wake wa 700 wakati Manchester City wakiwakaribisha Fulham Jumamosi na anatarajia kuiongezea idadi hiyo mara mbili yake kabla ya kustaafu.

Mhispania huyu akiwa kama msimamizi ameweza kufanya kazi katika nchi tofauti, akishinda mataji ya hadhi ya juu huko Uhispania, Ujerumani na Uingereza.

Kwa sasa anaendelea kulisaka taji lake la tatu la Ligi ya Uingereza huku kituo kinachofuata sasa ni kumenyana na mgeni wao Fulham.

Wenyeji watamkosa nyota wao Sergio Aguero ambaye ana shida ya goti  pale wanapokutana na timu ambayo wameifunga mara tisa mfululizo kwa tofauti ya magoli ya 27-3.

Guardiola amekuwa akiwanyanyasa na kuwatawala namna hiyo wapinzani wake wengi katika majukumu yake ya ukocha ambayo alianza akiwa na Barcelona B mnamo 2007, na ni matumaini yake safari yake ya soka bado ni ndefu.

“Michezo mia saba! Nitafikisha700 mingine zaidi kisha nistaafu. Sikutarajia.” – Guardiola

“Ni vizuri kuwa na michezo 700 huku ukiwa na vipigo vichache katika michezo hii, kwa wachezaji wote na wafanyikazi tuliokuwa nao katika Barca B, kikosi cha kwanza, Bayern [Munich] na hapa.”

“Ni idadi kubwa, na watu wote tulifanya vitu vya kushangaza kwa umoja na tunatumai tunaweza kufanya zaidi katika siku zijazo.”

Katika mechi zake 699 hadi leo, Guardiola ameonja ushindi mara 506 na kupoteza 82 tu kati ya hizo, akimwacha na ushindi mzuri wa asilimia 72.4.


 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Guardiola, Safari ya Guardiola Kufikia Mechi 700 Kama Meneja!, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa