Guardiola: Nasimama na Wachezaji Wangu

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kitu pekee anakifanya kwasasa ni kuhakikisha anawapa ushirikiano wachezaji wake kwa kuwapa moyo kutokana na kipindi kigumu ambacho wanapitia klabu hiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Manchester City wanapitia kipindi kigumu kutokana kusuasua kwenye ligi ya Uingereza na michuano mingine ambapo klabu hiyo ilicheza michezo saba bila kupata matokeo ya ushindi, Huku wakifungwa michezo sita wakisuluhu mchezo mmoja pekee kwenye michezo hiyo saba ikiwa ni rekodi mbovu kwa klabu hiyo na kwa kocha Guardiola pia.

guardiola

“Suluhisho la matatizo yetu ni kukaa nyuma ya  wachezaji wangu na tutafanikiwa.”

“Lakini hawezekani sasa hivi, na nadhani itachukua muda mrefu kutokea…”

Licha kusema atawapa nguvu na kuwanunga mkono wachezaji wake kocha Pep Guardiola amekiri sio rahisi kwasasa na anaona itachukua muda kidogo, Hii inaonekana wazi kocha huyo anaona kama wanahitaji muda kidogo ili kurejea kwenye ubora wao ambao kila mmoja ameuzoea kwani klabu hiyo kupitia kipindi kigumu kama hichi ni jambo ambalo limewashtua wengi.

 

 

Acha ujumbe