Guardiola: Sitaki Kuondoka Man City ikiwa kwenye hali hii

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema hataki kuondoka ndani ya klabu hiyo ikiwa kwenye hali ambayo inapitia kwasasa kwani anaamini anaweza kuweka vitu sawa na timu hiyo ikarejea kwenye ubora.

Guardiola na klabu yake ya Manchester City amekua akipitia kipindi kigumu zaidi tangu aanze kufundisha mpira wa miguu kwani kwenye michezo kumi ya mwisho aliyoiongoza klabu hiyo amefananikiwa kushinda mchezo mmoja tu, Huku michezo saba akiambulia vichapo na kupata sare michezo miwili jambo ambalo limekua la kustaajabisha.guardiola

“Zaidi ya hapo, ningejuta kuondoka Man City sasa! Nisingeweza kulala, hata zaidi nikifikiria sasa naondoka katika hali hii… haiwezekani.”

“Iwapo watanifukuza, hilo linaweza kutokea, kama tutaendelea. Lakini kuondoka sasa?! Hakuna nafasi. Ikiwa Khaldoon hafurahii, wanaweza kufanya hivyo.”

Aidha kocha Guardiola licha ya kusema hawezi kuondoka ndani ya klabu hiyo katika wakati kama huu lakini ameweka wazi kua kama mabosi wa klabu hiyo wakiamua kumfukuza kutokana na kinachoendelea klabuni hapo wanaweza kufanya hivo, Lakini kwa upande wake ameshatanabaisha kwa upande wake hawezi kuondoka kuiacha klabu kwenye kipindi kigumu kama hichi.

Acha ujumbe