Guardiola, Ten Hag, Arteta Kuwania Kocha Mwezi Febuari

Kocha Pep Guardiola wa Manchester City, Erik Ten Hag wa Man United na Mikel Arteta wa Arsenal kuwania tuzo ya kocha bora wa mwezi Febuari kunako ligi kuu ya Uingereza.

Makocha hao wote watatu wamefanikiwa kufanya vizuri katika mwezi huu wa pili kutokana na kuziongoza timu zao kupata matokeo ya ushindi katika michezo ambayo vilabu vyao vimecheza ndani ya mwezi Febuari.guardiolaKocha Pep Guardiola amefanikiwa kuiongoza Manchester City kwenye michezo sita ndani ya mwezi wa pili, Huku akifanikiwa kushinda michezo mitano kati ya michezo hiyo huku akisuluhu mchezo mmoja pekee dhidi ya klabu ya Chelsea.

Kocha Erik Ten Hag yeye kwa upande wake ameiongoza Man United katika michezo mitano ndani ya mwezi huu na kufanikiwa kushinda michezo minne, Huku wakipoteza mchezo mmoja wikiendi iliyomalizika dhidi ya klabu ya Fulham.guardiolaKocha Mikel Arteta yeye ndio anapigiwa upatu wa kuchukua tuzo hiyo kwani ndani ya mwezi Febuari yeye ana ushindi wa asilimia 100, Kwani ameiongoza timu hiyo katika michezo minne na yote amefanikiwa kuibuka na ushindi tena ushindi mnene.

Acha ujumbe