Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameongea na waandishi wa habari na kuwajibu swali walilouliza kama anaweza kutetea taji la ligi kuu ya Uingereza na kocha huyo alijibu bila kusita kua wanaweza kutetea taji hilo.
Kocha huyo amewaeleza waandishi wa habari wanaweza kabisa kubeba taji la ligi kuu ya Uingereza kwa mara nyingine, Lakini kama wataimarisha kiwango walichoonesha dhidi ya Liverpool na Tottenham.Kocha Pep Guardiola anatambua ni ngumu kubeba ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, Lakini yeye anaamini wanaweza kurejea kutwaa ubingwa huo kama wataendelea walipoishia kwenye michezo miwili dhidi ya Tottenham na Liverpool.
Manchester City kwasasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa nyuma ya Arsenal na Liverpool, Jambo ambalo linatia wasiwasi kwa mashabiki wa klabu hiyo lakini kocha wa timu hiyo anaamini wanakwenda kubeba taji hilo tena.Manchester City wakifanikiwa kubeba ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu huu tena wanaweka rekodi mpya ya kubeba ubingwa wa ligi ya mara nne mfululizo, Hii itakua ni rekodi ambayo haijawahi kufanywa hapo kabla chini ya kocha Pep Guardiola.