Mpango wa Liverpool kumsajili Marc Guehi unaweza kufufuka baada ya Manchester City kukumbwa na matatizo makubwa ya kisheria kufuatia kupatikana na hatia ya kuvunja sehemu kubwa ya kanuni za kifedha za Premier League.
City inakabiliwa na uwezekano wa kushuka daraja iwapo rufaa yake haitabadilisha uamuzi wa awali, hali ambayo inaweza pia kuwalazimisha mastaa kadhaa kuondoka Etihad. Iwapo City itashuka daraja, Guehi anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa kwenye rada ya klabu nyingine, huku Liverpool ikitajwa kuwa tayari kufufua mpango wa kumsajili beki huyo.

Liverpool iliwahi kushindana na City katika harakati za kumsajili Guehi, lakini City ikaibuka mshindi na kumnasa. Sasa, kwa mujibu wa Football Insider, mpango wa Guehi kwenda Anfield unaweza kuwa umerudi ikiwa City itakumbana na kushuka daraja.
Mick Brown, aliyewahi kuwa skauti wa Premier League, amesema kuna uwezekano mkubwa Liverpool ikarudi tena kwenye mbio za kumsajili Guehi iwapo City itashushwa daraja. “City ikishushwa daraja, itakuwa vigumu kuwabakiza wachezaji. Wanataka kucheza kwenye kiwango cha juu, Premier League na Champions League,” Brown alisema.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Brown ameongeza kuwa hali hiyo inaweza kuiweka City kwenye hatari ya kupoteza baadhi ya nyota wake muhimu, akiwataja Erling Haaland, Rayan Cherki na Ruben Dias pamoja na wengine.

Kwa upande wa Guehi, Brown amesema Liverpool inaweza kutumia nafasi hiyo kurejea kwenye mpango wake wa zamani. Liverpool iliripotiwa kuvutiwa sana na beki huyo na huenda ikajaribu kumleta Anfield iwapo mazingira yatabadilika.
Hata hivyo, Liverpool siyo klabu pekee inayoweza kufuatilia hali hiyo. Brown amesema klabu mbalimbali kutoka England na Ulaya zinaweza kuwa macho, zikisubiri kuona hatima ya City na uwezekano wa kuwapata baadhi ya wachezaji wake. Pamoja na hofu ya kuondokewa na mastaa, taarifa nyingine zinaeleza kuwa City bado ina matumaini ya kuwabakiza baadhi ya wachezaji wake wenye uzoefu hata kama klabu itashuka daraja.
Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi Pete O’Rourke, kushuka daraja kunaweza kusababisha fire sale Etihad, huku wachezaji kadhaa wakitarajiwa kupokea ofa nyingi za kuondoka. Hata hivyo, City inaamini baadhi ya wachezaji wake wakubwa wanaweza kubaki na kusaidia klabu kuanza upya.

Kwa sasa, hatima ya Guehi na wachezaji wengine wa City itategemea zaidi matokeo ya rufaa na hatua zitakazofuata katika sakata la kifedha. Ikiwa mazingira yatabadilika, Liverpool inaweza kuwa miongoni mwa klabu zitakazofuatilia kwa karibu nafasi ya kumsajili Guehi.


