Klabu ya Newcastle United imemuongezea mkataba kiungo wake raia wa kimataifa wa Brazil Bruno Guimaraes mkataba wa miaka mitano ambapo atasalia klabuni hapo mpaka mwaka 2028.
Kiungo Bruno Guimaraes amekubali kuongeza kandarasi ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2028, Huku kiwango cha kumuachia kiungo huyo ni paundi milioni 100.Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil amekua akionesha ubora mkubwa tangu atue klabuni hapo mwezi Januari mwaka 2022, Jambo ambalo liliwavutia klabu hiyo na kuamua kua nae kwa muda mrefu zaidi.
Kiungo huyo baada ya kuongeza mkataba anasema anajiskia furaha kuwepo ndani ya timu hiyo, Kwani tangu siku ya kwanza ametua ndani ya timu hiyo mashabiki wa klabu hiyo walimuonesha upendo wa hali ya juu ambao hajawahi kuuona klabuni hapo.Klabu yeyote ambayo itamtaka Bruno Guimaraes inapswa kwenda na kiasi cha paundi milioni 100 ili kuweza kumpata, Kwani ndio kiwango cha kumpata kilichojumuisha kwenye mkataba wake mpya vilabu kadhaa vilikua vinawinda saini ya kiungo huyo kama klabu ya Real Madrid.