Nahodha wa Newcastle United, Bruno Guimaraes, ameonyesha hisia kali baada ya kuitwa kwenye kikosi cha Brazil kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026, akisema sasa yuko tayari kuiishi ndoto kubwa akiwa na taifa lake.

Kiungo huyo alikosa nafasi kwenye kikosi kilichopita kutokana na majeraha, lakini sasa amerejea rasmi kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji 26 iliyotajwa na Carlo Ancelotti. Hii itakuwa mara yake ya pili kushiriki Kombe la Dunia baada ya kufika robo fainali na Brazil mwaka 2022 nchini Qatar.
Katika miaka ya hivi karibuni, Guimaraes amekuwa mmoja wa viungo muhimu zaidi ndani ya Seleção. Uwezo wake wa kukaba, kupandisha mashambulizi na kucheza nafasi tofauti umemfanya kuwa mchezaji anayeheshimika sana na Ancelotti, ambaye aliwahi kusema kuwa Bruno ni mchezaji kamili na mwenye mchango mkubwa kwa timu ya taifa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Baada ya kuitwa kwenye kikosi hicho, Guimaraes aliandika ujumbe wa hisia kwenye Instagram uliowagusa mashabiki wengi. Aliikumbuka safari yake tangu akiwa mtoto akienda kutazama mechi akiwa na wazazi wake kwenye viwanja vya Rio de Janeiro, hadi kuondoka nyumbani akiwa mdogo kwenda kufukuzia ndoto zake São Paulo.

Nyota huyo pia aliwashukuru wazazi wake kwa kumuamini na kumuacha aishi ndoto yake, safari iliyompeleka kupitia Athletico, Lyon, Newcastle hadi timu ya taifa ya Brazil. Sasa akiwa mmoja wa viongozi wa kizazi kipya cha Brazil, Guimaraes anaamini muda umefika wa kupigania ndoto kubwa zaidi, kuiletea Brazil utukufu mwingine wa dunia.


