Unapomzungumia Erling Braut Haaland, unazungumzia vilabu vitatu (kwa sasa), ni jukumu lake kuamua hatma yake msimu ujao.

Kimkataba, Haaland anaweza kuondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu. Hili litawezekana kwa klabu yeyote itakayolipia ada ya £63M ambayo ipo kwenye mkataba wake na klabu hiyo.

Japokuwa, hii haimaanishi kuwa BVB hawawezi kumbakiza klabuni hapo. La Hasha! BVB wanaweza kumshawishi mshambuliaji huyo kubakia Signal Iduna Park. Kwa hali ilivyo, Dortmund wanakwama kwenye hesabu zao sokoni.

Manchester City inaripotiwa kufikia makubaliano ya awali na Haaland na kwamba, City wanajiandaa kulipa pesa inayotakiwa kumsajili mchezaji huyo. Hakuna majadiliano na BVB, ni suala la kulipa pesa iliyopo kwenye mkataba wake tu.


Haaland

Pamoja na City, Real Madrid wanatajwa kwenye kinyang’anyiro hiki. Japokuwa, kwa Madrid kuna tatizo kidogo. Uongozi wa klabu hiyo haufikirii kufanya usajili wa mchezaji yeyote ambaye matakwa yake ya mshahara, yanawezakuondoa usawa wa mishahara kwa wachezaji wao. Kwa sababu hii, kuna uwezekano wakaachana na Haaland na kusajili mshambuliaji wa aina nyingine.

Mpaka sasa, Erling mwenyewe hajatoa neno la maamuzi yake. Wakati vilabu hivi vikiendelea kusikika maskioni mwa mashabiki wa soka, jibu sahihi na uhalisia upo mikononi mwa Erling peke yake. Ataamua hatma yake yeye mwenyewe.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa