Haaland Mbioni Kumpita Messi, Rekodi Mbili Ziko Hatarini

Erling Haaland ameendelea kuonyesha kuwa yuko kwenye kiwango cha kuvunja rekodi baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa Manchester City wa 2-0 dhidi ya Porto kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League.

Haaland Mbioni Kumpita Messi, Rekodi Mbili Ziko Hatarini

Brace hiyo imefikisha idadi ya mabao yake kwenye mashindano hayo hadi 59, sawa na aliyowahi kufunga Andriy Shevchenko. Haaland alianza safari yake ya Champions League akiwa Salzburg, akafunga 15 akiwa Borussia Dortmund, kabla ya kuendeleza kasi hiyo akiwa Manchester City.

Sasa akiwa na miaka 26, Haaland yuko bao moja tu kufikia mabao 60 ya Champions League. Lakini bao hilo moja linaweza kumweka kwenye historia kwa kuivunja rekodi ya Lionel Messi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufikisha mabao hayo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Haaland Mbioni Kumpita Messi, Rekodi Mbili Ziko Hatarini

Messi alifikisha bao lake la 60 akiwa na miaka 26 na siku 86, katika mchezo wake wa 80 wa Champions League. Haaland kwa sasa ana miaka 26 na siku 50, hivyo ana nafasi moja kubwa ya kumpita Muargentina huyo.

Mchezo unaofuata wa City kwenye Champions League ni dhidi ya Paris Saint-Germain Oktoba 14, siku ambayo Haaland atakuwa na miaka 26 na siku 85, siku moja tu akiwa mdogo kuliko Messi alipofikisha bao la 60.

Kufunga dhidi ya PSG hakutakuwa kazi rahisi kama ilivyokuwa dhidi ya Porto, lakini ukiwa na Haaland hakuna kinachoweza kuonekana hakiwezekani. Na hata akikosa kuvunja rekodi hiyo ya umri, bado ana nafasi kubwa ya kumpita Messi kwenye rekodi nyingine.

Haaland Mbioni Kumpita Messi, Rekodi Mbili Ziko Hatarini

Haaland amefikisha mabao 59 katika mechi 59 tu za Champions League, wakati Messi alihitaji mechi 80 kufikisha idadi hiyo. Hivyo, Haaland ana nafasi ya kutumia hadi mechi 20 zaidi kuvunja rekodi ya Messi, au 21 ili kuifikia kwa idadi sawa ya mechi.

Nyota huyo wa City tayari anashikilia rekodi ya kufikisha mabao 50 ya Champions League kwa idadi ndogo zaidi ya mechi. Sasa bao la 60 linasubiri na kwa kasi aliyonayo, inaonekana ni suala la muda tu kabla historia nyingine haijaandikwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.