Earling Haaland nyota wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund anakwenda kukutana na waajiri wake hao wa zamani katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya ambapo kwasasa yeye ataitumikia klabu ya Manchester City.

Nyota huyo wa huyo aliitumikia miamba hiyo Ujerumani kwa misimu miwili kwa ubora mkubwa akitokea klabu ya Red Bull Salzrburg leo ataenda kuvaana na timu hiyo katika dimba la Etihad ambapo klabu ya Manchester City ikiwa nyumbani.

earling haalandHaaland amekua katika kiwango kizuri tangu kujiunga na klabu hiyo kutoka jijini Manchester akiwa tayari amefunga magoli 12 katika mechi za kimashindano ambapo tayari ana goli kumi katika mechi sita za ligi kuu ya Uingereza na magoli mawili katika mchezo mmoja aliocheza wa ligi ya mabingwa dhidi ya klabu ya Sevilla wiki ilopita katika dimba la Ramon Sanchez Pizjuan.

Kitu kikubwa kinachosubiriwa katika mchezo huo ni namna gani nyota huyo ataendeleza ubora wake na kuweza kuwaadhibu waajiri wake hao wa zamani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa