Haas : Kevin Magnussen Mbadala wa Nikita Mazepin.

Timu ya Haas imethibitisha kurejea kwa Kevin Magnussen katika timu hiyo kwa msimu wa Formula 1 wa 2022 kufuatia kufutwa kazi kwa dereva Mrusi Nikita Mazepin.

 

Timu hiyo inayomilikiwa na Marekani ilisitisha mkataba na Mazepin baada ya kupata shinikizo kubwa la kuchukua hatua kufuatia uvamizi wa nchi yake nchini Ukraine, huku michezo duniani ikikata uhusiano na Urusi.

Magnussen, ambaye ametia saini makubaliano ya mkataba wa muda mrefu, alikua Haas kwa misimu minne kabla ya timu hiyo kumwachia mwishoni mwa kampeni ya 2020.

Dereva huyo wa Denmark sasa anarejea kwa mkataba wa muda mrefu wakiungana pamoja na mjerumani, Mick Schumacher msimu utakapoanza nchini Bahrain mnamo Machi 20.

Mchezaji wa Akiba wa Brazil Pietro Fittipaldi atafanya majaribio na timu ya Haas nchini Bahrain siku ya Alhamisi kufuatia kuondoka kwa Mazepin.

Timu ya Haas ilimaliza ya mwisho mwaka wa 2021 na ndiyo timu pekee ambayo haikupata pointi baada ya kupambana kutengeneza gari lao kwa ajili ya mabadiliko makubwa ya kanuni za mwaka huu.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe