'Hakuna Haja ya Kumuwahisha Thiago Alcantara'

Nyota huyu raia wa Hispania ameshindwa kuwepo dimbani kwa zaidi ya miezi miwili sasa tangia alipopatikana na jeraha la goti kwenye debi ya Merseyside dhidi ya Everton mwezi Oktoba.

Nyota huyu pia alipatikana na maambukizi ya Corona, kitu kilichomfanya akose mechi nyingi zaidi. Amecheza mara mbili tu akiwa na klabu ya Liverpool tangia alipowasili klabuni hapo kutokea Bayern Munich.

Thiago Alcantara
Thiago Alcantara

Staa huyu wa miaka 29 amerejea kufanya mazoezi na kikosi kizima cha timu ya Liverpool mapema Jumatano. Hata hivyo, kwa mujibu wa Klopp, kumchezesha kwenye mechi ijayo, ya Jumapili dhidi ya West Brom bado itakuwa ni mapema sana kwa nyota huyu kurejea dimbani.

Klopp anaamini Xherdan Shaqiri na James Milner wanaweza wakarejea na kuwa msaada wakati, Thiago Alcantara akiendelea kusubiri.

“Thiago tayari ameshapiga hatua moja katika mazoezi ya timu. Bado hajaanza kujumuishwa moja kwa moja kwenye mazoezi kwa ujumla lakini ameanza kupiga hatua nzuri, kwa bahati mbaya baada ya mda mrefu, hatuwezi na hatutamuwahisha.”

– Klopp akizungumzia hatua ya kutejea kwa Thiago Alcantara


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

13 Komentara

    Liver kafika

    Jibu

    Ni vzur pia

    Jibu

    Bado mashabiki tunamkubali

    Jibu

    Ni vizuri

    Jibu

    Tunamkubali sana mashabiki

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Pole Sana

    Jibu

    Goodnews

    Jibu

    Ni vizuli

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Ni vizuri ili kusaidia Thiago Alcantara aweze kurudi kwenye fomu yake

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Kama amepona acheze tu

    Jibu

Acha ujumbe