Manchester City imefanikiwa kung’ara kwenye tuzo za ulaya jioni ya leo jijini Monaco ambapo mshambuliaji wa klabu hiyo Earling Haaland na kocha Pep Guardiola wote wakiibuka na tuzo.
Mshambuliaji Earling Haaland amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora barani ulaya ambayo alikua akigombea na mchezaji mwenzake wa Man City Kevin de Bruyne pamoja na Lionel Messi, Huku Pep Guardiola yeye akitwaa tuzo ya kocha bora wa ulaya.
Tuzo hizi zimekwenda sehemu husika kwani mshambuliaji huyo aliisaidia klabu yake ya Manchester City kutwaa kombe la ulaya mwezi wa sita mwaka huu, Vilevile kocha Pep Guardiola alifanikiwa kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la ulaya.
Mshambuliaji Earling Haaland mbali na kuisaidia Man City kutwaa taji la ulaya lakini pia alifanikiwa kumaliza kama mfungaji bora wa michuano hiy akiwa na mabao 12, Lakini pia akiwa amemaliza kama mfungaji bora wa ligi bora tano ulaya.
Kocha Pep Guardiola yeye ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka wa ulaya sio kwasababu tu ya kuisaidia Man City kutwaa taji la ulaya, Lakini pia akiandika rekodi ya kuisaidia City kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja na kuivunja rekodi ya majirani zao Man United.


