Haller Kurejea Uwanjani Tena

Mchezaji wa zamani wa Ajax na sasa Borrusia Dortmund Sebastian Haller ameshangazwa na “huruma” ya watu wengine tangu agundulike ana saratani ya korodani, huku rais wa FIFA Giann Infantino akimuunga mkono mshambuliaji huyo kurudi uwanjani.

 

Haller Anatarajia Kurejea Uwanjani

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alijiunga na Dortmund katika kampeni mpya, baada ya kuwa na msimu mzuri 2022/2023 akiwa Ajax na kumfanya kama mfungaji bora wa Eredivisie.

Mipango yake ya kuleta matokeo mapema uwanjani nchini Ujerumani ilivurugika wakati uvimbe ulipopatikana, huku mchezaji huyo wa zamani wa Westham mwenye umri wa miaka 28 akihitajika kufanyiwa Chemotherapy.

 

Haller Anatarajia Kurejea Uwanjani

Haller amekuwa akieleweka kwa kusita kurejea uwanjani, lakini anahisi mawazo chanya kutokana na maendeleo anayofanya huku akisema:

“Mimi ni mzima sana. Matibabu yanendelea vizuri, na kwa bahati nzuri ninaweza kufanya mazoezi kila siku”

Akizungumzia uungwaji mkono ambao amekuwa nao, Haller aliiambia FIFA.Com:”Ilikuwa ni mshtuko lakini sasa ni chanya. Sikutarajia kupata jibu kama hilo au kuwa na huruma nyingi kwangu, na sio kutoka kwa ulimwengu wa kandanda haya ni mambo ambayo yanatuleta sote pamoja, na yamenipa kiasi kikubwa cha nguvu katika kukabiliana na changamoto hii.

Haller Anatarajia Kurejea Uwanjani

 

“Haijalishi ni raia wa Ivory Coast, Uholanzi, Kifaransa, Kijerumani, Kiingereza au chochote, kila mtu ambaye amenipa msaada kutoka karibu au mbali ni chanzo cha nguvu  kwa familia yangu, marafiki na mimi.

Haller aliongezea kwa kusema kuwa anajitahidi kwa kadri awezalo ili aweze kurudi uwanjani  na kuchukua jukumu kwa klabu na nchi yake, ambapo alijitokeza uwanjani kushudia timu yake hiyo ikicheza kwenye michuano ya klabu bingwa UEFA dhidi ya Copenhagen ambapo timu yake ilishinda kwa mabao 3-0.

Dalili zinaonyesha kuwa kuna matumaini ya yeye kurudi uwanjani kucheza atakapokaa sawa ambapo mkuu wa FIFA alimwandikia kuwa,

 

Haller Anatarajia Kurejea Uwanjani

“Kwa niaba ya mimi binafsi na jumuiya ya kimataifa ya soka, ningependa kutoa matakwa yangu ya dhati kwako kwaajili ya kupona kabisa na haraka, na ninatumai kukuona ukirejea  katika afya njema hivi karibuni”.

Acha ujumbe