Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane amegoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo na anataka kuondoka kwenye timu hiyo.
Harry Kane mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu na klabu ya Tottenham lakini klabu yake inahitaji kumuongezea mkataba mchezaji huyo, Huku upande wa mchezaji ukiwa hauhutaji kuongeza mkataba na klabu hiyo.Mchezaji huyo amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Tottenham na kumfanya kutajwa kama moja ya washambuliaji bora kwasasa barani ulaya, Huku akifanya vilabu mbalimbali barani ulaya kupigana vikumbo kuhitaji saini yake.
Harry Kane kama klabu ya Tottenham itamzuia kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, Itamfanya mchezaji huyo kuondoka bure klabuni hapo kwakua hana mpango wa kusaini mkataba mpya ndani ya Spurs.Mshambuliaji Harry Kane anatajwa kutaka kutimkia klabu ya Bayern Munich ambao wameshatuma ofa mbii ndani ya klabu ya Spurs ambapo mwanzo Manchester United ndio walikua wanaongoza kwa kwenye mbio hizo lakini kwasasa wamehamishia nguvo zao kwa raia wa Denmark Rasmus Hojlund.