Harry Kane : Chaguo Langu Lilikua Bayern

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga klabu ya Bayern Munich Harry Kane amesema klabu hiyo anayoitumikia kwasasa ndio lilikua chaguo lake baada ya kuamua kua ataondoka Tottenham.

Mshambuliaji Harry Kane aliulizwa na mwandishi wa habari juu ya kuhitajika na Man United kwenye dirisha kubwa lililopita na akabainisha kua vilabu vingi vilimuhitaji lakini yeye aliamua kuichagua Bayern Munich.harry kaneNahodha huyo wa timu ya taifa ya Uingereza ameyazungumza hayo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya makundi dhidi ya Manchester United.

Inafahamika kua Manchester United ilikua ni moja ya vilabu vilivyokua vinaonesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, Lakini walishindwana kutoka na bei ambayo Totenham walihitaji kwa mchezaji huyo.harry kaneLicha ya Harry Kane kuzungumza leo klabu ya Bayern Munich ilikua ndio chaguo lake, Lakini vyanzo vinaeleza kua mshambuliaji huyo alikua yupo tayari kujiunga na Man United dirisha lililopita kabla ya United kushindwana na Tottenham kwenye bei.

Acha ujumbe