Harry Kane hatasaini mkataba mpya na Tottenham huku Bayern Munich wakionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29.
Harry Kane ambaye ni nahodha wa Uingereza hana haraka ya kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto lakini inawaacha Tottenham wakikabiliwa na uamuzi wa kumwacha au kujaribu kushinda taji au kufuzu Ligi ya Mabingwa wakiwa naye katika kikosi chao msimu ujao.
Bayern Munich wametoa ofa ya pauni milioni 68 kwa Harry Kane lakini Tottenham wamempa thamani ya pauni milioni 100.
Endelea kutumia Meridianbet kufanya ubashiri wa mechi mbalimbali na michezo ya kasino ya mtandaoni itolewayo kama vile Poker, Aviator, Roullette na mingine kibao.
Gazeti la Daily Mail linasema kuwa Tottenham imewataja wachezaji wawili ambao wanaweza kuchukua nafasi ya kiungo Pierre-Emile Hojberg, ambaye huenda akahamia Atletico Madrid. Mchezaji chipukizi wa Chelsea Conor Gallagher na Douglas Luiz wa Aston Villa wametambuliwa kama chaguo linalowezekana.
West Ham inaendelea kutafuta kuziba pengo la Declan Rice, ambaye alijiunga na Arsenal wiki iliyopita, imetua kwa James Ward Prowse wa Southampton, Guardian inaripoti. The Hammers wako tayari kumruhusu Flynn Downes kwenda Southampton ikiwa na maana wanaweza kumpata Ward-Prowse mwenye miaka 28.
Birmingham Live imesema Aston Villa wamefanikiwa kuinasa saini ya winga wa Ufaransa Moussa Diaby kutoka Bayer Leverkusen.