Harry Kane Kutokipiga Dhidi ya Brazil

Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane hatafanikiwa kukipiga katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa leo baina ya timu yake ya taifa dhidi ya timu ya tiafa ya Brazil.

Harry Kane yupo kwenye sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza lakini amepata majeraha madogo ambayo yatamfanya kukosa mchezo wa leo dhidi ya mabingw amara tano wa dunia timu ya taifa ya Uingereza.harry kaneTaarifa za kukosekana kwa mshambuliaji huyo kwenye mchezo wa leo amezitoa kocha wa timu hiyo Gareth Southgate ambaye ameeleza Kane hataweza kuwepo kwenye mchezo wa leo kutokana na majeraha ambayo yanamkabili.

Mshambuliaji huyo amekua mchezaji wa kutumainiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza, Lakini kwenye mchezo mkali wa leo dhidi ya Brazil atakosekana japo kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza bado kina washambuliaji wengine wazuri ambao wanaweza kucheza nafasi hiyo.harry kaneNdani ya kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza wamebaki washambuliaji watatu ambao wanaweza kuvaa viatu vya Harry Kane na kucheza vizuri kwenye nafasi hiyo ambao ni Jarrod Bowen, Ollie Watkins, pamoja na Ivan Toney na jukumu linabaki kwa kocha Southgate kuamua anaanza na nani katika mchezo huo.

Acha ujumbe