Nyota wa Harry Kane anatajwa kuwa ataruhusiwa kuondoka Tottenham Hotspurs ikiwa malipo yatakuwa ni taslimu pekee.

Nyota huyu wa miaka 27 amekuwa akihusishwa zaidi na kuondoka London Kaskazini, huku kukiwa na nia ya kumsajili kutoka vilabu vya Manchester City, Chelsea na Manchester United.

Kwa mujibu wa The Sun, City walikuwa wanajiandaa kuwatoa Raheem Sterling na Gabriel Jesus, pamoja na £60m kwa ajili ya kuwashawishi Spurs kumuuza Harry Kane. Hata hivyo, Daniel Levy anataka zaidi ya £150m kwa ajli ya nahodha huyo wa Uingereza na watapokea pesa pekee.

Harry Kane

Levy anatazamia kuboresha kikosi chake baada ya kuwa na msimu wa kusuasua wa 2020-21, ambayo iliwashuhudia wakimaliza nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi.

Licha ya Raheem Sterling na Gabriel Jesus kuwa wanaweza kuwa wachezaji muhimu kwa Spurs, kwa kuzingatia mafanikio yao wakiwa na City, bado kukubali dili la kubadilishana kutawafanya City kukosa pesa ya kutosha kuwekeza kwenye usajili wa msimu wa joto.

Vilabu vyote, Chelsea na Man United vinaripotiwa kuwa tayari vimekuwa kwenye mazungumzo na wakala wa Harry Kane kwa miezi ya hivi karibuni, lakini maamuzi juu yake yanatarajiwa kufanyika baada ya Euro 2020.


 

WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa