Nahodha wa klabu ya Manchester United Harry Maguire amesama hana nia ya kuachia kitambaa cha unohodha wa timu hiyo licha ya kuwa na kiwango kibovu kwenye msimu ulioisha.

Kocha mpya wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesithibitisha kuwa Harry Maguire ataendelea kuwa nohadha wa timu hiyo, licha ya kuwa mashabiki wengi wa timu hiyo kutaka mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Uingereza kunyanganywa unahodha.

Harry Maguire

Harry Maguire alikuwa sehemu ya safu ya ulinzi wa klabu ya Manchester ambayo iliruhusu magoli 57, kwenye michezo ya ligi kuu ya Uingereza, magoli manne zaidi ya kuliko timu ambayo imeshuka daraja ya Burnley.

Harry Maguire alikubali kuwa msimu ulioisha hakuwa na kiwango kizuri, lakini hayuko tayari kuachia kitambaa cha unahodha. “Sikiliza, msimu uliosha ulikuwa sio mzuri kwangu, Maguire alimwambia mwandishi. “Kama mimi sikucheza vizuri na kama timu hakika hawakucheza vizuri.

“Lakini karia nzuri inaweza kuwa kwa miaka 10 hadi 15, na huwezi kuwa na kipindi kizuri kila mwaka na kutokuwa na kipindi kigumu.

“Unapaswa kupambana, hupaswi kuangalia mambo ya nyuma na mwaka uliopita hakika ni historia kwenye karia yangu. Lakini imekwisha sasa tunaangalia mbele kwa ajiri ya kuirudisha klabu sehemu iliyokuwepo, hicho ndicho kipaumbele sasa.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa