Mchezaji wa klabu ya Manchester United Harry Maguire amepokea kitisho cha kutumiwa bomu nyumbani kwake siku ya jumatano na polisi wameanza kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Siku ya leo polisi mchana na mbwa maalum amabao wanawauwezo wa kutambua milipuko walifika nyumbani kwa Maguire, ambapo anaishi yeye na mchumba wake, Fern Hawkins na wanawe wawili.

Harry Maguire
Harry Maguire

Msemaji wa familia ya Harry Maguire alisema, “ndani ya saa 24 zilizopita, Maguire alipokea kitisho cha hatari nyumbani kwake, ma ameshatoa taarifa hii polisi ambao waanafanyia kazi hili swala. Usalama wa familia yake na maeneo yote yanayomzunguka ni kipaombela namba moja kwa Maguire.

“Ataendelea kujiandaa na mchezo wake wa wikiendi dhidi ya Arsenal kama kawaida na kwa sasa hatuta zungumza neno lolote kwa wakati huu.”

Waraka wa Polisi wa Cheshire ulieleza, “siku ya jumatano 20 April, kituo cha polisi cha Cheshire tulipata taarifa ya kuwepo kitisho cha bomu kwenye anwani ya eneo la Wilmslow. hakuna mtu yeyote aliyehamisha lakini kwa tahadhari polisi walikwenda na mbwa maalum kwenda kukagua na eneo lote linalozunguka.”

Harry Maguire amekuwa muhanga wa kupokea vitisho kutoka kwa mashabiki uwanjani na kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kiwango chake msimu huu.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa