Jina la beki la pembeni Mtanzania anayekipiga Klabu ya Nkana ya nchini Zambia, Hassan Kessy, limejadiliwa na Kamati ya Usajili ya Yanga na kukabidhiwa kwa Kocha Mkuu Mbelgiji, Luc Eymael huku Kessy mwenyewe akisisitiza kuwa yupo tayari kujiunga Yanga.
Kessy ni kati ya wachezaji wanaotajwa hivi sasa kuwaniwa na Yanga katika kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambao timu hiyo imepanga kukisuka kikosi chao ili kichukue makombe.
Beki huyo ni mchezaji huru hivi sasa kwa mujibu wa kanuni za Fifa kutokana na mkataba wake kumalizika Agosti, mwaka huu, hivyo anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine itakayomhitaji.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, Yanga inataka kumsajili beki huyo kwa ajili ya kuiboresha safu hiyo ya beki ya pembeni inayochezwa hivi sasa na Juma Abdul na Paul Godfrey ‘Boxer’ ambaye hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kocha ndiye aliyependekeza usajili wa beki wa pembeni katika kuiboresha na Kessy ndiye aliyependekezwa na baadhi ya viongozi wa Yanga.
Aliongeza kuwa jina la Kessy tayari limekabidhiwa kwa kocha ambaye yeye ataamua asajiliwe au vipi, hivyo kama akikubali basi haraka atapewa mkataba wa miaka miwili.
“Kessy ndiyo jina la kwanza la beki wa kulia lililopendekezwa na mabosi wa Yanga ambao tayari wamempatia kocha ambaye yeye ndiye atakayeamua hatima yake.
“Kocha anamtaka beki mwenye uwezo na uzoefu wa kucheza michuano ya kitaifa na kimataifa, hivyo upo uwezekano mkubwa wa Kessy kusajiliwa na Yanga,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Kessy kuzungumzia hilo alisema: “Mimi mkataba wangu unatarajiwa kumalizika mwezi Agosti, hivyo nipo tayari kujiunga nayo kwani nimepata taarifa za kunihitaji, lakini bado hawajanifuata kiofisi.”
Ernest
Hapa yanga wanatakiwa wasipoteze muda kama Kessy alikuwa kwenye kiwango kizuri basi ni wakati wa kumjumuisha kwenye kikosi chao ili kuleta upinzani
Lydia Emmanuel Magoti
Safii Sana habari nzuri
Issa
Kessy yanga ni safi kurudi huko ulipokua kama kumedumaza kiwango chako
Omary lukumbi
Safi sana wachangamkie fursa hyo fasta
Shafii
Kama angekua yupo kwenye form nzuri nkana ya Zambia ingemuongezea mkataba hamna kitu hapo.
Edgar
Karbu sana nyumbn Ni nyumbn
Saupha mohamed
Bora aluji ajekuikomboa yangaa maana mmmh
Gabriel
Ni habar njema sana kwa mashabiki wa yanga kuona bek wetu amerud tena kufanya Kaz kwan Tanzania kwa ujumla tunatambua uwezo wake
Baada ya kuonyesha uwezo mkubwa, uongozi wa Moro Kids kama kawaida yao ulifanya mazungumzo na wenzao wa Mtibwa Sugar kwa lengo la kumsajili Kessy kwenye timu yao ya vijana ili kuanza kupata uzoefu.
Mtibwa Sugar walimsajili Kessy msimu wa 2011 aliitimikia timu hiyo hadi mwaka 2014, ndipo Simba walipomuona baada ya kucheza mechi ya Ligi Kuu ambayo kocha Mecky Mexime alimtumia na kuonyesha kiwango kikubwa.
Alitua Simba msimu wa 2014 kwa mkataba wa miaka miwili ambapo, hakupata changamoto ya namba kwani aliyekuwepo kwa wakati huo, Emiry Nimubona, raia wa Burundi hakuwa kwenye kiwango bora.
Msimu wa mwisho mwa 2016, Kessy alijiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ambao, ulimalizika mwaka jana, 2018 na kujiunga Nkana Rangers ya Zambia inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili. Akiwa Nkana ameshiriki michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.
Hivyo tunatarajia tena kumuona kujiunga na club ya wananchi
Furahav
Itakuwa vizuri km akirudi yanga.
sabrina
Imekaapoa hii
Franky
Jabari njema sana izii
Hope mwaikuka
Arud tu nyumban
MnonganeJR
Habari njma kwa mashabiki Wake pamoja & yanga afrika#
Povel tz
Arud tu nyumban nafas yake ipo pale Jangwan
Njiku
Acha arudi aokoe jahazi maana yanga hawapo sawa
Aziza mushi
Arudi tu
JULIANA
Kweli TZ tunavipaji sawa akuje tu yanga
Amiri Kayera
Kalb mwamba
Evaluziga
Rudi bwana maana yanga inakaribia kufa kabisa
Magdalena
Hana jipya Tena uyo angekuwa ni mahili nkana wangeendelea kubaki nae yanga nao wanasajili tu ovyo wanabidi ndo timu itakuwa imara kumbe wanapoteza
Izo pesa wanazozitumia kusajili watu ni Bora wangewapatia wachezaji waliopo Ili wapate moyo wa kucheza kwa juhudi zote
Magdalena
Hana jipya Tena uyo angekuwa ni mahili nkana wangeendelea kubaki nae yanga nao wanasajili tu ovyo wanadhani ndo timu itakuwa imara kumbe wanapoteza
Izo pesa wanazozitumia kusajili watu ni Bora wangewapatia wachezaji waliopo Ili wapate moyo wa kucheza kwa juhudi zote
Dorophina
Inabidi yanga wasipoteze muda kumsajili kiungo huyo katika kikosi chao
Samiah
Nihabari njema
Khadija
Karibu sana kwani nyumbani ni nyumbani#meridianbettz
Adelta
Ni habari njema
Mwanahamisi
Habari njema kwa mashabiki wake
Sylvester
Yanga inahitaji nafkiri kukisuka kikosi chake chote namaanisha kwenye idara zote kwani timu haipo vizuri kabisa,Kessy kurudi nae atakuja kuwasaidia sana
Elika
Natumai wana yanga watakuwa wameipokea vizur hii habari…hongera kwao wana yanga
felister
fursa iyo
Ester jackson
habar njema sana kwa mashabiki wa yanga kuona bek wetu amerud tena kufanya Kaz kwan tuna matumaini kuwa kikosi chetu kitakuwa imara zaidi ukiangalia kwa hasaivi tunategemea kupata wachezaji wa nnje wa 5 wa ndani 4 ambao wanajua mpinda wa kimataifa ambao wanaweza kuisuka yanga ikawa iko katika kiwango kizuri zaidi .
Genia Sikaluzwe
Habari njema kwa mashabiki wa nyanga kupata beki mzuri na mwenye viwango vya juu
lombo
saf
isha
Arudi tuu maana wanayanga wako vibaya kwakweli
Zeiyana
Karibu tena yanga hassan kesi mashabiki wa simba wataongea sana lakini kwa vile wew mwenyew hunaonesha bado damu yako hipo yanga mtoto kurudi kwao sio mbaya naona wengi hawajui umetokea wapi wanaongea ongea tu
Angelina
Habari njema kwa mashabiki wa yanga
David Pere
Nalo ni Jambo zuri Kama atarudi ili kuiokoa timu take ya zamanii
Fatuma kasomo
Habari nzuri kwa yanga
Salma
Habari njema
devotha
habari njema bora arudi kuisaidia yanga
Theonestina
Saafi sana
Sadick
Kama Nkana hawajaonyesha nia ya kuendelea nae inawezekana hana kiwango cha kutisha. Timu zetu zinapaswa kusajiri watu watakaoleta mafanikio katika timu#meridianbettz
Saupha mohamed
Aludi kuisaidia yanga
caroline
asije akazingua kama Morrison
mwakalosi
huyu ana nin mbona anapenda shida jaman
Rehema
Hii ni habari njema