HATMA YA NGOMA MIKONONI MWA FADLU

UONGOZI wa Klabu ya Simba SC inasubiri ripoti ya Kocha Fadlu Davids ili kumaliza hatima ya Kiungo Fabrice Ngoma katika klabu hiyo hivi karibuni

Ngoma anataka mkataba wa miaka miwili na Simba SC wamesisitiza hawatampa ofa hiyo bali wapo tayari kumpa mkataba mpya wa mwaka mmoja tu.

Simba SC inasubiri maamuzi ya mwisho ya Kocha ili kufanya uamuzi wa kumbakiza Ngoma kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi au kuachana nae.

Acha ujumbe