Eden Hazard ameomba radhi kwa mashabiki wa Real Madrid baada ya kuonekana akicheka na wachezaji wa Chelsea kufuatia timu yake kuondolewa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano.

Hazard Aomba Radhi kwa Kutaniana na Wachezaji wa Chelsea

Mchezaji huyo wa Ubeligiji ambaye alitumia miaka saba huko Stamford Bridge kabla ya kijiunga na Madrid mwaka 2019, alikosolewa vikali baada ya kuonekana akitaniana na wachezaji wenzake wa zamani.

Alicheza kwa dakika 89 katika mchezo walipoteza kwa 2-0 huko London magoli ya Timo Werner na Mason Mount yalitosha kabisa kuwapeleka Chelsea fainali ambayo watamenyana na Manchester City.

Lakini wachezaji wengi wa zamani wa Real Madrid walimtaka Hazard kuomba radhi kwa mashabiki kwa kuonesha kitendo hicho.

Na Hazard siku ya Alhamisi ilimbidi afanyie kazi ushauri huo kwa kuandika ujumbe uliyosomeka: “Samahani, nimesoma maoni mengi kuhusu mimi leo lakini haikuwa kusudio langu kuwakera mashabiki wa Real Madrid.

“Siku zote nilikuwa na ndoto ya kuichezea Real Madrid na nilikuja hapa kushinda, msimu bado haujaisha kwa pamoja lazima tupiganie LaLiga! Hala Madrid!”


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Hazard, Hazard Aomba Radhi kwa Kutaniana na Wachezaji wa Chelsea, Meridianbet

SOMA ZAIDI

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa