Hazard Kuikosa Mechi Nyingine ya Real Madrid!

Changamoto ya majeraha inaendelea kumtesa Eden Hazard Uhispania.

Huu umekuwa msimu mwingine mgumu kwa nyota Eden Hazard, ambaye anapambana kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Carlo Ancelotti.

Hazard ameanza kwenye gemu 4 pekee za La Liga msimu huu, na amekuwa akikosolewa juu ya kiwango chake uwanjani.

Hivi karibuni kulikuwa na tumaini huenda akaimarika na kuongeza ushindani kikosini, lakini suala la majeraha bado limemkumbatia staa huyu.

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Staa huyu mwenye miaka 30 sasa, bila shaka alikuwa anatamani kuwa na kumbu kumbu nzuri na Real Madrid, amezikosa safari tatu za ugenini za hivi karibuni kwa sababu ya changamoto ya misuli.

Kwa mujibu wa COPE, Hazard ataikosa gemu ya Jumatano dhidi ya Athletic Club kwa sababu ya majeraha.

Licha ya changamoto kuonekana kutokuwa kubwa, ni kikwazo kingine kwa staa huyu ambaye alikuwa na ndoto ya kufanya vyema huko La Liga, baada ya kutawala EPL akiwa na The Blues.


 

MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe