Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson amekutwa hana hatia katika shutma za ubaguzi ambazo alikua anakabiliwa nazo. Baada ya uchunguzi kufanyika na shirikisho la mpira nchini Uingereza FA limebaini mchezaji huyo hana hatia.

Wiki mbili zilizopita katika mchezo uliozikutanisha klabu za Liverpool na klabu ya Arsenal kulitokea mzozo baina ya Henderson na beki wa Arsenal Gabriel, Na ikitajwa kua mchezaji huyo alimbagua beki huyo mwenye asili ya weusi.hendersonKutokana na tukio hilo shiri8kisho la mpira wa miguu nchini Uingereza FA likafanya uchunguzi kubaini kama hizo shutma ni za kweli kwa kiungo huyo wa kiingereza. Baada ya uchunguzi kukamilika imebainika hakukua na ubaguzi wa aina yeyote uliooneshwa.

Kiungo Henderson amefanikiwa kutoka salama katika tuhuma hiyo ambayo shirikisho hilo imekua ikikemea kwa kiwango kikubwa na kusisitiza uungwana michezoni.hendersonBaada ya hukumu hiyo kutoka wadau wengi wameonesha kutokuridhishwa na kuamini kua nahodha huyo alifanya vitendo vya kibaguzi lakini kama shirikisho limeamua kumtetea.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa