Gwiji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Barcelona na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry, Amezungumza kua anatamani kumuona mchezaji mwezake wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Zinedine Zidane akiifundisha timu hiyo.henryZidane toka aondoke ndani ya Real Madrid umepita takribani mwaka mmoja sasa, na amekua akihusishwa na vilabu tofauti tofauti lakini mpaka kufikia sasa hajajiunga na klabu yeyote ambaye amekua akihusishwa nayo.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal wakati anafanya mazungumzo na chombo kimoja cha habari hivi karibuni akiulizwa kuhusu Zidane kujiunga na Juventus ” Zidane amekua akihusishwa na vilabu kadhaa na hajajiunga na hata kimoja kati ya hivo. Na nafikiri sidhani kama anataka hizo kazi. Namuuona Zidane akisubiria kibarua cha timu ya taifa ya Ufaransa na itakua chagua sahihi kwake” Alisema HenryhenryGwiji Henry anaamini moja kwa moja Zidane anasubiri ofa ya kua kocha wa timu ya taifa ya ufaransa ndo maana amekataa ofa ya vilabu mbalimbali baada ya kutimka ndani ya Madrid mwaka 2021.

Zidane bingwa mara tatu mfululizo wa ligi ya mabingwa ulaya inaelezwa ndoto yake kubwa ni kurudua mafanikio aliyoyapata na timu ya taifa ya Ufaransa kama mchezaji kuja kuyapata kama kocha wa timu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa