Higuain Aanza Vibaya Inter Miami.


Gonzalo Higuain, 32, alipoteza mkwaju wa penalti katika mchuano wake wa kwanza ndani ya jezi za kikosi cha Inter Miami inayomilikiwa na mwanasoka wa zamani wa Manchester United, David Beckham.

Inter Miami walipokezwa kichapo cha 3-0 na Philadelphia Union katika mechi hiyo ya Major League Soccer (MLS) mnamo Septemba 27, 2020.

 

Higuain Aanza Vibaya Inter Miami.

Higuain ambaye ni raia wa Argentina, alisajiliwa na Inter Miami mnamo Septemba 18, 2020 baada ya mkataba wake na Juventus ya Italia kutamatishwa.

Nyota huyo ambaye pia amewahi kuvalia jezi za Chelsea, alipaisha penalti aliyoaminiwa kupiga katika dakika ya 77.

Mechi hiyo ilikamilika kwa hisia kali baada ya Higuain kuzua vurugu kwa kumsukuma beki Jakob Glesnes aliyesherehekea bao la Philadelphia mbele yake.

 

Higuain Aanza Vibaya Inter Miami.

Ingawa hivyo, kocha wa Inter Miami, Diego Alonso alieleza kuridhishwa na mchango wa Higuain katika mechi hiyo na kusisitiza kwamba mchezaji huyo atayaweka kando maruerue ya kupoteza penalti na kujipanga katika mechi zijazo.

Mabao ya Philadelphia yalifungwa na Anthony Fontana, Ilsinho na Brenden Aaronson.

Inter Miami kwa sasa wanashikilia nafasi ya 13 kwenye msimamo wa MLS Tawi la Mashariki kwa alama sawa na DC United. Philadelphia wanakamata nafasi ya pili kwa alama mbili pekee nyuma ya viongozi wa msimamo, Columbus Crew.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

35 Komentara

    Kiukweli walianza vinasa sana inatakiwa wakae wayajutie makosa aliyoyafanya higuan

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Higuain pole sana ila usikate tamaa bado muda upo ongeza juhudi

    Jibu

    Higuain pole sana

    Jibu

    kuanza vibaya si kumalizia vibaya, anaweza akaanza vibaya na mwisho wa siku akamalizia vizuri

    Jibu

    Inter Jana walipoteza mechi kwa uzembe wao walikuwa wanakosa magoli ya wazi kabisa

    Jibu

    Inter jana walianza vibaya kweli ila bado wana nafasi yakufanya vuzuri

    Jibu

    Poleni sana Higuain

    Jibu

    Poleni ila msikate tamaa!

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

    Duu pole yake nyota huyo msimu kuwanza vibaya

    Jibu

    Higuain ameaza mchezo vibaya kwanza kukosa penat pili kutaka kuanzisha fujo ugenini asipoangali anaweza kuwekwa bench na club yake

    Jibu

    Poleni sana inter ila kuteleza sio kuanguka

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Pole san inter

    Jibu

    Higuani anatakiwa kutulia tuu

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

    Bahati akiuwa yao

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Pole sana 💗

    Jibu

    Duuh pole sana

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Higuan anatakiwa kutulia

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Mwanzo mgumu!!

    Jibu

    Mpila umeisha akubali alud Argentina

    Jibu

    kuanza vibaya si kumalizia vibaya, anaweza akaanza vibaya na mwisho wa siku akamalizia vizuri

    Jibu

    Pole sana Higuain.

    Jibu

    Hayo ndio maisha ya mpira wanatakiwa wakubaliane na matokea tu

    Jibu

    Jamanii

    Jibu

    Duh majanga

    Jibu

    anaweza akaanza vibaya na mwisho wa siku akamalizia vizuri

    Jibu

    Duuh

    Jibu

Acha ujumbe