Timu ya taifa ya Hispania leo itajitupa uwanjani kumenyana na timu ya taifa ya Morocco katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa kombe la dunia. Mechi hiyo itakayopigwa katika dimba la Education City nchini Qatar.

Mechi hiyo ambayo itawakutanisha mshindi wa kwanza wa kundi F na mshindi wa pili wa kundi E ambapo mchezo huo utaamua ni nani kwenda kwenye hatua ya robo fainali kwenye fainali hizo za mwaka 2022.hispaniaTimu ya taifa ya Hispania hii inakutana na Morocco na mechi hii inakua ni mechi ya majirani kwani kutoka nchini morocco na kufika Uhispania ambapo ni bara ulaya kabisa ni karibu mno na inakadiriwa ni umbali wa kilomita 1331. Hii inaonesha ni kwa namna gani kuna ukaribu nchi hizo zina ukaribu.

Timu ya taifa Hispania ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu kutokana na ubora wanaounesha kwenye michezo yao chini ya mwalimu wa zamani wa klabu ya Barcelona Luis Enrique.hispaniaTimu ya taifa ya Morocco wao wanachukuliwa kama timu ambayo inaweza kushangaza wengi kwani kwenye hatua ya makundi walifanikiwa kuongoza kundi lenye vigogo kama Croatia na Ubelgiji. Timu hiyo imeonesha ubora wa hali ya juu kwenye hatua za makundi hivo Uhispania maarufu kama La roja wanapewa tahadhari juu ya timu ya taifa ya Morocco.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa