Hodgson Ajiuzulu Kama Kocha wa Palace Kufuatia Ugonjwa

Roy Hodgson amejiuzulu wadhifa wake kama mkufunzi wa Crystal Palace huku klabu hiyo ikiwa juu kwa pointi tano tu kutoka eneo la kushuka daraja la EPL.

Hodgson Ajiuzulu Kama Kocha wa Palace Kufuatia Ugonjwa

Huku kukiwa na uvumi unaoongezeka kwamba The Eagles walikuwa wamempanga Oliver Glasner kuchukua nafasi yake, kocha huyo mkongwe, mwenye miaka 76, alipelekwa hospitalini wiki iliyopita baada ya kuugua wakati wa mazoezi.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Palace, alisema: “Klabu hii ni ya kipekee sana na ina maana kubwa kwangu na imechukua sehemu kubwa katika maisha yangu ya soka. Nimefurahiya sana wakati wangu hapa kwa misimu sita kwani imenipa nafasi ya kufanya kazi na wachezaji wa kiwango cha juu na wafanyikazi wa kufanya kile ninachopenda kila siku.”

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa, inapenda kumshukuru Steve Parish na washirika wake wa Marekani kwa msaada wao, pamoja na wakufunzi wake na timu ya nyuma ambao wamemsaidia sana njiani.

Hodgson Ajiuzulu Kama Kocha wa Palace Kufuatia Ugonjwa

“Shukrani na heshima yangu pia kwa kikosi cha sasa cha wachezaji ambao wamekuwa na furaha kufanya kazi nao. Ni sifa kwa klabu na wao wenyewe. Nina hakika mashabiki wetu wataendelea kutoa sapoti yao kamili kwa timu kwa muda uliosalia wa msimu huu na zaidi.”

Ray Lewington na Paddy McCarthy watachukua usukani kwa mchezo wa leo usiku huko Everton

Palace, ambao wamethibitisha kuwa Hodgson ameruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri, wanashika nafasi ya 16 kwenye ligi kabla ya mtanange wa leo usiku dhidi ya Everton.

Hodgson Ajiuzulu Kama Kocha wa Palace Kufuatia Ugonjwa

McCarthy na Lewington wataiongoza timu katika uwanja wa Goodison Park, huku mbadala wa kudumu wa Hodgson akitarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Acha ujumbe