Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Rasmus Hojlund amefanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa wiki wa ligi ya mabingwa ulaya.
Rasmus Hojlund anaingia kwenye kinyang’anyiro hicho kutoka na kuonesha kiwango bora katika wiki hii ya ligi ya mabingwa ulaya, Mchezaji huyo alifanikiwa kufunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Galatasaray licha ya klabu yake kupoteza mchezo.Mchezaji huyo ameungana na wachezaji wengine kama Jude Bellingham wa klabu ya Real Madrid, Alvaro Moratta wa Atletico Madrid, pamoja na mshambuliaji wa klabu ya Braga Bruma.
Wachezaji wote wanne wameweza kuonesha ubora mkubwa katika michezo ya timu zao ambapo Jude Bellingham alihusika na mabao mawili akifunga bao moja na kupiga pasi moja ya bao, Morrata yeye alifunga mabao mawili, Bruma alipiga pasi moja ya bao na kufunga moja, Rasmus Hojlund yeye alifanikiwa kufunga mabao mawili.Mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Denmark mpaka sasa ana mabao matatu kwenye ligi ya mabingwa ulaya, Mabao mawili ya juzi yalimfanya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa wiki wa ligi ya mabingwa ulaya wakati huo timu yake ikiwa inashika mkia kwenye kundi lake wakiwa hawana alama hata moja.