Licha ya kuhusishwa na vilabu kama Arsenal, Juventus na PSG, tulishuhudia Houssem Aouar akibaki Olyimpique Lyonnais kwa msimu mwingine.

Uwezo wake wa kutawala safu ya kiungo ni kati ya vitu vikubwa alivyonavyo kiungo huyu wa Lyon na Timu ya Taifa ya Ufaransa.

Tukiangalia hali ya sasa kwa vilabu vilivyokuwa vinaiwania saini yake, haipishani sana na hali ya Lyon licha ya kwamba timu hiyo haichezi Ligi ya Mabingwa msimu huu baada ya kumaliza katika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Ligue 1 msimu uliopita.

Akizungumza na RMC, Houssem Aouar amesema “sioni inawezekanaje nikose furaha kwenye mji wangu, klabu yangu [Lyon]. Ni kitu ambacho sikielewi. Ninafurahi kuwepo hapa, niliamua kubaki kwenye klabu yangu. Ninachokitaka ni kuiweka timu hii kwenye nafasi yake, nikishirikiana na wachezaji wenzangu.

“Tunamalengo makubwa msimu huu. Ninaongea sana na uongozi wa klabu pamoja na kocha, ulikuwa ni wakati wa kawaida tu [kuhusishwa na vilabu vingine].”


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Houssem Aouar, Houssem Aouar Hajutii Kubaki Lyon, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa