Mwamuzi wa zamani kutokea nchini Uingereza ambaye alishawai kuchezesha fainali ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini na michuano ya ulaya 2010 Howard Webb anatarajia kuchukua nafasi ya Mike Riley kama kiongozi wa waamuzi kwenye Premier League.

Howard Webb ambaye anatambulika kama moja waamuzi bora sana hasa kwenye kipindi chake baada ya kufanya kazi bora sana kwenye ligi kuu nchini Uingereza na kupelekeka kupewa kuongoza michezo mikubwa sana barani ulaya na duniani.

Howard Webb, Howard Webb Kurejea Uingereza Kama Boss, Meridianbet

Howard Webb kwa sasa anajiandaa kuacha kazi kwenye ligi kuu ya Marekani Major League Soccer, ambayo ameitumika kuanzia mwaka 2018 kama mkuregenzi wa waamuzi kwenye ligi hiyo, na kwenda kuchukua nafasi hiyo nchini Uingereza kama mkurengenzi ambapo atambulika kama  ‘PGMOL’.

Ilitangazwa mwezi june, kwamba kiongozi wa waamuzi, Mike Riley, ataachia ngazi baada ya kuongezeka kwa msukumo wa viwango vya waamuzi kuwa chini na waamuzi wa VAR kutokuwa na maelewano mazuri kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Howard Webb akizungumza kuhusu majukumu yake mapya alisema: “Ninashauku ya kurejea nchini Uingereza na kuanza changamoto mpya nitakapomaliza majukumu yangu ya mkataba na PRO, ni nafasi nzuri kwangu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa