Chama cha soka Afrika Kusini (Safa) imemtangaza Hugo Broos (69) 🇧🇪 kuwa kocha wa Bafana Bafana 🇿🇦. Kocha huyo anatarajiwa kutua Southa Afrika wiki ijayo kwaajili ya kuanza kibarua cha kuinoa timu hiyo.

Hugo amesaini kandarasi ya miaka 5 na mshahara wake unakadiriwa kufika Tsh 115m kwa mwezi. DR Congo walikua wanajiandaa pia kumtangaza lakini alibadili mawazo baadae.

 

hugo, Hugo Broos Kocha Mpya Bafana Bafana., Meridianbet

“South Africa ina utajiri wa historia katika mpira wa miguu na ni moja ya timu kubwa duniani” Hugo aliiambia tovuti ya Chama cha soka Afrika kusini (Safa).

“Nchi ina vipaji vingi na nimekuja kufundisha taifa lenye mpira halisi na uwezo mkubwa.

“Lengo langu kubwa litakuwa kuandaa wachezaji wapya ambao wana njaa na hamu ya mafanikio. Wachezaji wachanga wana tamaa na wanataka kudhibitisha hilo.

“Ninahitaji kuanza kutoka hapo kwa sababu nataka kujenga kikosi chenye nguvu cha Bafana Bafana kwa siku zijazo. Hii ni project ya kusisimua na nimefurahi sana. “

Hugo anachukua nafasi ya Molefi Ntseki ambaye alifutwa kazi mwezi machi baada ya Bafana Bafana kushindwa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

hugo, Hugo Broos Kocha Mpya Bafana Bafana., Meridianbet

SOMA ZAIDI

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa