Timu ya taifa ya Hungury imeedelea kushangaza wadau wengi wa soka baada ya kuendelea kufanya vizuri katika michuano ya Uefa Nations League inayoendelea kwasasa.

Hungury mpaka sasa wamefanikiwa kukaa kileleni kwenye kundi la 3 ambalo lilionekana kua gumu sana kwa upande wao likijumuisha timu za Italia,Uingereza, pamoja na Ujeruma lakini timu hiyo imefanikiwa kuongoza kundi hilo wakiwa na alama kumi.

hunguryVijana hao wa kocha Marco Rossi wameshinda michezo mitatu,wamesuluhu mchezo mmoja na kufungwa mchezo mmoja kitu ambacho kimeendelea kuwashangaza watu wengi kwani hawakua wakipewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye kundi hilo lenye miamba ya soka barani ulaya.

Ujerumani wakiwa nyumbani wamepokea kipigo kutoka kwa timu hiyo usiku wa kuamkia leo na kuendelea kudhihirisha licha ya kutopewa nafasi ya kufanya chochote ila wao wanaonesha wanaweza kufanya lolote dhidi ya mpinzani yeyote.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa