Ibrahim Ajibu Aungana na Zahera Coastal

Mchezaji wa zamani wa vilabu vya Simba, Yanga na Azam Ibrahim Ajibu amefanikiwa kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Coastal Union kuelekea msimu ujao.

Ibrahim Ajibu amefanikiwa kujiunga na kocha wake wa zamani ndani ya klabu ya Yanga Mwinyi Zahera ambaye kwasasa amejiunga na klabu ya Coastal Union.Ibrahim ajibuCoastal Union wanajiandaa kufanya vizuri kuelekea msimu wa 2023/24 ambapo msimu uliomalizika walikua kwenye hatari ya kushuka kitu ambacho kinaonekana hakikuwafurahisha viongozi wa klabu hiyo.

Kiungo huyo amejiunga na klabu hiyo kutoka mkoani Tanga kwa uhamisho huru kutoka Singida Fountain Gate zamani Singida Big Stars ambapo alisaini mkataba wa mwaka mmoja na kumalizika msimu uliomalizika.Ibrahim ajibuKiungo Ibrahim Ajibu wengi wanamtabiria kufanya vizuri ndnai ya Coastal Union kwani katika maisha yake ya soka alicheza kwa kiwango bora zaidi akiwa chini ya kocha Mwinyi Zahera ambae anaenda kuungana nae ndani ya klabu hiyo ya Wanamangushi.

 

Acha ujumbe