Mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa ‘Ligue 1’, Paris Saint-German wamefanikiwa kumbakiza kikosini nyota wa timu ya taifa ya Argentina, Mauro Icardi na kumsainisha mkataba wa miaka minne. Dili hilo litamfanya Icardi aendelee kubaki PSG mpaka June 2024!
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina aliyeitumikia PSG tangu mwezi wa tisa mwaka jana akiwa kama mchezaji wa mkopo kutokea Inter Milan, ameonesha kiwango cha kuridhisha ndani kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, na tayari amefanikiwa kuingia katika muunganiko mzuri uliozaa utatu mtakatifu wa Yeye (Icardi), Neymar na kylian Mbappe kiasi cha kutosha kuwashawishi mabosi wa PSG kutoa kitika cha zaidi ya pauni 54m ili kuinasa saini yake.
Hapo awali iliripotiwa kuwa PSG wangetakiwa kutoa zaidi ya pauni 60m ili kumsajili jumla nyota huyo katika kikosi chao, lakini hilo limekwamishwa kutokana na matokeo ya mlipuko wa janga la Corona na athari zake katika uchumi wa vilabu mbali mbali duniani.
Mauro Icardi mwenyewe anaonesha kuwa na furaha ndani ya PSG na mara kadhaa amenukuliwa akikiri hilo, sio tu na waandishi wa habari lakini pia na waliokuwa mabosi wake akiwa Inter. “Yeye (Icardi) anataka kuendelea kubaki PSG, sisi kama timu tupo katika mazungumzo ili kufanikisha hilo”, alinukuliwa Piero Ausilio, mkurugenzi wa michezo wa Inter Milan akisema kabla dili hilo halijakamilika.
Mpaka sasa nyota huyo wa Argentina ameshacheza jumla ya mechi 31 na kikosi cha PSG huku akiingia kambani mara 20! Icardi amekuwa mbadala sahihi kabisa wa nyota Edinson Cavanni aliyekuwa akiandamwa na majeraha.


mathayo sonje
ningeshangaa kama PSG wangemuondoa kikosin Icard, hili pia ni jembe ambalo linamsaada sana pale PSG
David pere
Kama kweli atabaki PSG itatisha sanaa msimu ujao
mwakalosi
huu ni uamzi mzuri kwa Icardi maana kutokuelewana na maboss zake wa zamani pale international Milan hakukuwa na afya kwa kazi yake
Hamidu
Icard mchezaji amestahili kupewa mkataba wa kudumu hapo PSG#meridianbettz
Povel
Ni maamuz mazur sana kumbakiza kwn icardi kwn cavan hatambulik Kama hatasalia thnks kwa update za michezo na burudani
Lombo
Icardi amejtaid kwa kiasi chake
Mwajuma
Maamuzi mazuri kubaki PSG maana ataangeenda Inter angekaa benchi tu wakati Icardi nimchezaji mzuri sana
Shafii
Safi Sanaa
Gabriel
Kutokana na icardi kuenyesha uwezo wake PSG wanastahil kumfanya abaki tu coz anamchango mkubwa sana
Ernest
Icardi really deserve it.
dorophina
Psg ilitakiwa kumpa mkataba wa maisha icardi coz Ni mchezaji mzuri sana
Emmy cleopa
Safii sana
Hidaya Mohammed
Icardi ndio jembe la PSG
Amani
Dili hilo litamfanya Icardi aendelee kubaki PSG
Lydia Emmanuel Magoti
Ikopoa Kama kweri atabaki PSG itatisha Sana msimu unaho kuja huo
Maleek Jigga
PSG wataendelea kutisha Ligue 1
Caroline
PSG bila Icardi hakuna kitu
Magdalena
Icard yupo poa Sana na kaipa jina PSG
Genia Sikaluzwe
Icardi kwa Psg ni sehemu mzr kwake .magoli 20 kwa mechi 30 ni jinsi gani anavyoonesha kwamba anastaili kubaki
Mwanaidi
Aendelee kubaki sababu ni mchezaji mahiri sana na PSG inamuamini sana
Elika
Jembe hilo libakie tu psg
Rehema Dickson
uamzi mzuri kwa Icardi maana kutokuelewana na maboss zake wa zamani pale international Milan hakukuwa na afya kwa kazi yake
Hope mwaikuka
Abak Psg tu
Salma
Abaki PSG kwana anaipenda kutoka moyoni nafikili msimu unao kuja atafanya maajabu makubwa
Antony Luseno
PSG imefanya maamuzi mazuri
Juliana
Bwana mtu asikwambie kizuri kizuri tu, Icardi mchezaji hodari
Ester jackson
Mauro Icardi mwenyewe anaonesha kuwa na furaha ndani ya PSG amefanya kitu kinzuri sana nimeipenda hii
Evaluziga
Dili hilo litamfanya lcardi aendelee kubaki PSG
felister
Icardi anastahili ongera kwa ofa ya mkataba mrefu
Theckla
Icardi anajua mpira
Aziza mushi
Akibaki psg watatisha Sana msimu ujao.
Kenani
Kwa kocha mwelev uwez kumluhusu atoke kwa kipind hiki
Rehema
Abaki hapo hapo
Samiah
Abaki hapo hapo👊
Asha mvugalo
Hongera sana.