IDDI NADO ATOA KAULI YA KIBABE

NYOTA wa Azam FC, Idd Suleiman Nado ameweka wazi kuwa malengo makubwa ni kuona kwamba wanatwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu mpya wa 2024/25 kutokana na maandalizi mazuri ambayo wanayafanya kwa sasa.

Azam FC chini ya Kocha Mkuu Yusuph Dabo imeweka kambi Morocco ikiwa ni mwendelezo wa kuelekea msimu mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.iddi nadoIkumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Azam FC iligotea nafasi ya pili kwenye msimamo vinara walikuwa ni Yanga walimaliza wakiwa na pointi 80 kibindoni.

Iddi Nado amesema: ” Kwa sasa mahitaji makubwa ni kuona kwamba ninanyanyua kwamba kwa kutwaa mataji na hilo linawezekana kutokana na maandalizi mazuri ambayo tunayafanya. Ndondo nimechukua sana huko nimechukua huko yote Mazenze na nani ila sasa nikichukua hili la Ligi Kuu na CRDB Cup.

“Msimu uliopita sikufanya vizuri kuwa kuwa nilitoka kufanyiwa upasuaji nikarejea uwanjani hivyo nilishindwa kuwa kwenye mwendezo mzuri. Nina amini kwamba msimu ujao utakuwa bora na wenye ushindani.”

Acha ujumbe