Iheanacho aweka rekodi mpya EPL 2020/2021

Wakati mbwa mwitu wa Uingereza Leicester City ikipokea kipigo cha 2-1 dhidi ya Chelsea, Mchezaji Iheanacho alikuwa mfungaji pekee wa goli la kufuatia machozi la Leicester City akipokea pasi kutoka kwa mnigeria mwenzake Wilfred Ndidi.

Katika mechi iliyoonekana kuwa na ugumu kwa upande wa Leicester ambao lango lao lilikuwa likishambuliwa kama nyuki na vijana wa Tuchel, Iheanacho aliweka rekodi ya kuwa mfungaji pekee kufunga katika kila siku ya mechi ya EPL msimu huu. Goli la jana linamfanya Iheanacho kuwa na jumla ya magoli 12 msimu huu.

Chelsea walikuwa butu sana katika eneo la ushambuliaji, wakiwa na mashuti 16 huku wakilenga lango mara 4 tu! Huku goli moja alilofunga Timo Wener likikataliwa na VAR baada ya kukutwa kwenye mtego wa Offside.

Magoli ya Rudiger na lile la penati lililofungwa na Jorginho yalitosha kupeleka ushindi Stamford Bridge na kuwafanya Chelsea kujikusanyia alama tatu muhimu kuwasaidia kusalia Top 4 Msimu huu.

Dakika sita tu zilimtosha Kelechi Iheanacho kuonesha makali yake baada ya kuingia dakika ya 70 kufuatia kutolewa kwa Maddison na goli likawarudisha mchezoni. Lakini bahati haikuwa kwao na wakaambulia kipigo hicho.

Matokeo hayo ya jana yanaweka Chelsea nafasi ya 3 wakiwa na alama 67, huku Leicester City akienda nafasi ya 4 akiwa na alama 66 na Liverpool nafasi ya 5 wakiwa na alama 63 na mchezo mmoja mkononi ambao watacheza na Burnley leo.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

BASHIRI SASA

Acha ujumbe