Infantino Ataka Kila Nchi iupe Uwanja Jina la Pele

Rais wa shirikisho la soka duniani Gianni Infantino ameomba kila nchi duniani mwanachama wa shirikisho hilo iweze kuupa uwanja jina la gwiji wa soka duniani Pele.

Gwiji Pele ambaye amefariki wiki iliyopita anapewa heshima kubwa sana na wadau wa mpira wa miguu duniani kutokana na namna ambavyo ameutumikia mchezo huo, Gwiji atazikwa ndani ya wiki hii huko kwao Brazil kwenye makaburi ya Ghorofa.infantinoRais Infantino amesema kua kila nchi ingependeza kama ingeupa jina la Pele kwenye moja ya viwanja vinayopatikana kwenye nchi husika ili kumuenzi gwiji huyo, Aliyasema wakati wa shughuli ya kuuaga mwili wa gwiji huyo hapo jana katika jiji la Santos ambapo ndio sehemu ambayo Pele amecheza mpira kwa muda mrefu zaidi.

Gwiji Pele anashikilia rekodi ya kua mchezaji ambaye ameshinda mataji mengi ya kombe la dunia akiwa ameshinda mataji matatu mwaka 1958,1962, na 1970, Huku pia akiwa hajawahi kupoteza fainali yeyote kwenye michuano hiyo kwani kila fainali aliyocheza amefanikiwa kushinda.infantinoRais Infantino anasema anaheshimu mchango wa Pele kwenye mpira wa miguu na gwiji huyo anahitaji heshima ya aina yake, Na yeye akaomba kila nchi iupe walau uwanja mmoja jina la gwiji huyo kutokana na makubwa ambayo ameyafanya kwenye mpira wa miguu.

Acha ujumbe