Nyota wa zamani wa Barcelona na timu ya Spain, Andres Iniesta ameongeza mkataba wa Miaka miwili kuendelea kuchezea timu ya Vissel Kobe ya Japan.
Kufanya hivyo kutamfanya mspain huyo kuendelea kucheza soka mpaka atakapokaribia kuwa na mika 40. Iniesta alisaini mkataba huo mpya katika siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 37.
Toka ajiunge na Vissel Kobe, Andres amefanikiwa kuisaidia timu yake kuchukua kombe la mfalme na Japanese Super Cup. Iniesta amecheza mechi 77 huku akifunga magoli 16 na kutoa pasi za magoli 18 katika michezo yote.
Itakumbukwa kuwa Iniesta aliondoka Barcelona mwaka 2018 akiwa miongoni mwa viungo wa kati bora sana duniani na alikuwa na huzuni sana kuagana na klabu hii.
Mchezaji huyu nguli wa soka, alitoka Barca akiwa amecheza mechi 674, huku akifunga magoli 57, kutoa assisti 139 na kushinda jumla ya makombe 30 na Klabu hiyo. Vilevile, Andres alishinda kombe la dunia na kombe la Euro akiwa na Spain mara mbili.
Bila shaka umri ni namba tu, cha muhimu ni ujuzi usioweza kuisha na Japan wanaendelea kufurahia huduma ya mchezaji huyu nguli sana katika ulimwengu wa soka.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
aisha
Big up kwake
Johnmary jo
Hongera sana zidi kuongeza bidii
Venerose
Hongera sana
Sarah
Ongera kwake
Magdalena
Safi sana
Mariam mtandama
Safi
Mwanahamisi
Hongera kwake
Lydia Emmanuel Magoti
Safii sana
Amiri Kayera
Saf