Inter Milan Wamgeukia Edinson Cavani

Klabu ya Inter Milan imevutiwa na mshambuliaji wa klabu ya Manchester United ambaye mkataba wake na mashetani wekundu unakwenda kuisha mwezi june kama mbadala wa Alexis Sanchez.

Inter Milan wanatafuta mashambuliaji ambaye anaweza kuongeza hamasa ya safu ya ushambuliaji kwenye timu hiyo, kwa sababu mchezaji Sanchez anaweza kuruhusiwa kuondoka mwishoni mwa msimu.

Inter milan

Cavani amefunga magoli mawili tu kwenye michezo 17 aliyoicheza klabu ya Manchester United msimu huu, majeruhi yamekuwa kikwazo kwake msimu, huku msimu uliopita akifunga magoli 17 kwenye michezo 39 aliyocheza akiwa na jezi ya mashetani wekundu.

Barcelona nao wamehusishwa na taarifa za kuhitaji huduma mshambuliaji huyo mwenye miaka 35, huku wakiwa na matumaini kuwa wanaweza kumshawishi kuweza kumwaga wino kwenye klabu hiyo.

Wachezaji wengine ambao wanahusishwa na klabu ya Inter Milan ni Luis Suarez wa Atletico Madrid na Dries Mertens wa Napoli.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe