Inter Milan bado wana uhakika wa kumsajiri mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Romelu Lukaku kwa uhamamisho wa mkopo wa muda mrefu Lakini bado mpaka sasa wapo kwenye meza ya mazungumzo kuhusu uhamisho huo.

Leo mapema, mkurugenzi muendeshaji wa klabu ya Inter Milan Alessandro Antonello, alithibitisha kuwa Lukaku alimwambia kuwa anahitaji kurudi kwenye klabu katika dirisha la majira ya kiangazi msimu huu, na anatumai kuwa wataweza kukubaliana Chelsea.

Inter Milan

“Hakika kuna shauku kubwa ya lukaku kurudi, mapitio ya kiuchumi ni radhima yathibitishwe na kuna maswala ya kiutaalamu inabidi yatatuliwe. Kuanzia June 30 tutajaribu kumsajiri ndani ya muda uliopangwa.” Alisema Alessandro Antonello

Chelsea hawana mpango wa kumtumia mshambuliaji wake Romelu Lukaku kwa msimu ujao, pia wanahitaji kupunguza mzigo wa mshahara na wanahitaji kiasi kidogo cha pesa kutoka kwa timu inayohitaji huduma yake.

Awali klabu ya Chelsea iliweka £24milioni, kabla ya kupunguza mpaka £10milioni, lakini Inter Milan wanataka kulipa £5milion ila wamekubali kulipa mshahara wake ambapo yeye mwenyewe amekubali kupunguza.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa