Inter Milan Wanaongoza Mbio Kumsajili Origi.


 

Inter Milan wanaongoza mbio za kumsajili Divock Origi kutoka Liverpool – kulingana na Calcio Mercato – Antonio Conte anataka kumsajili msaidizi Romelu Lukaku, ambaye amekuwa katika kiwango bora kwa kufunga mabao 15 katika mechi 17 msimu huu.

Wolves na Newcastle pia wamehusishwa na mshambuliaji huyo wa Kimataifa Ubelgiji, ambaye anaonekana kutaka kuondoka viunga vya Anfield katika mwaka huu mpya.

 

Inaaminika kuwa Majogoo nao wako tayari kuachana na shujaa wao wa Ligi ya Mabingwa Januari hii na wanasikiliza ofa kwa mshambuliaji huyo wakati Jurgen Klopp akitafuta pesa za kusajili beki.

Origi ataungana tena na raia mwenzake Romelu Lukaku ikiwa atajiunga na Inter Milan, ambao wanaangalia uwezekano wa mkataba wa mkopo.

Origi, aliyejiunga na Liverpool kwa pauni milioni 10 mwaka 2014 akitokea Lille na ana Mkataba hadi 2024, ni kipenzi thabiti cha mashabiki Anfield kwa misimu miwili iliyopita, lakini amecheza mara nane tu kwenye mashindano yote msimu huu.

 


JIUNGE NA FAMILIA YA MERIDIANBET BURE!!!!

Ndio, kwetu Mteja ni mfalme. Jiunge sasa na familia ya Meridianbet bila malipo yeyote na sisi tutakuzawadia bonasi ya shilingi 3,500 kama sehemu ya kukukaribisha kwenye familia hii BURE!!!. Unasubiri nini??

BOFYA HAPA

16 Komentara

    Safi Inter milan

    Jibu

    Noma sana inter

    Jibu

    Inter wakimpata huyo mchezaji itakuwa poa sana

    Jibu

    Safiii lnter

    Jibu

    Itapendeza kama watapata sain yake

    Jibu

    Vizuli sana lnter itapendeza

    Jibu

    Milan naona hawataki mchezo kabisa

    Jibu

    Vizuri san intermilan

    Jibu

    Fresh tu

    Jibu

    Wameamua kujipanga kiakili

    Jibu

    Itakuwa Deal zuri kwa Orig

    Jibu

    Orig jembe

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Wakaze buti tu

    Jibu

    Itapendeza

    Jibu

    Wakazane tu

    Jibu

Acha ujumbe